Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Julai, 2024
Arsenal wanakaribia kufikia dili la £25m kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real Sociedad. (Mirror)
West Ham wanakaribia kuwasajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, na fowadi wa Leeds wa Uholanzi Crysencio Summerville, 22. (Sky Sports)
Nottingham Forest hailengi kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Morgan Gibbs-White, 24, licha ya Newcastle, Arsenal, Aston Villa na Chelsea kutaka kumnunua. (HITC)
West Ham wamekubali masharti ya kibinafsi ya kumsajili beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka, 26, lakini bado hawajakubaliana ada na Manchester United, ambao wanataka £18m badala ya £10m iliyotolewa. (Sky Sports Ujerumani)
Fulham wapo kwenye mazungumzo ya hatua ya juu kumnunua beki wa kati wa Villarreal Mhispania Jorge Cuenca, mwenye umri wa miaka 24, kwa £6.7m. (Standard)
Napoli wana ofa ya euro 12m (£10.2m) tayari kwa kiungo wa kati wa Brighton na Scotland Billy Gilmour mwenye umri wa miaka 23 na wanasubiri wachezaji kuondoka katika klabu hiyo kabla ya kuitoa. (Sky Sports Italia)
Roma wamekubali mkataba na Girona kumsajili mshambuliaji wa Ukraine Artem Dovbyk, 27, kwa £28.8m - huku AC Milan ikionyesha nia ya kumsajili fowadi wa Roma wa Uingereza Tammy Abraham, 26. (Repubblica)
Stuttgart wataondoa nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brighton na Ujerumani Deniz Undav, 28, na kuangalia walengwa wapya hivi karibuni ikiwa hawawezi kufikia makubaliano na Albion. (Kicker)
Newcastle wapo kwenye hatua ya juu ya mazungumzo na Sheffield United ili kumsajili mshambuliaji wa Blades wa Denmark William Osula, 20 kwa dau la awali la £10m. (Telegraph)
Leipzig itakataa ombi la pili kutoka kwa Barcelona kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26. (Sport)
Aston Villa wamefikia makubaliano na Chelsea kumnunua mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anataka kujiunga na Napoli ya Antonio Conte. (Il Mattino)
![]() |
West Ham wapo ukingoni kusaini mikataba miwili, timu inayoshiriki Ligi Kuu ya England imefikia makubaliano ya kumsajili Romelu Lukaku na Arsenal wakaribia kumnunua Mikel Merino |
Arsenal, Real Madrid na Atletico Madrid wote wanamtaka kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Juventus. (Gazetta)
Kiungo wa kati wa Manchester City Muingereza Jacob Wright, 18, amekubali kuhamia Peterborough United kwa mkopo.
Bristol City, Stoke na Birmingham City wanavutiwa na mlinzi wa Burnley raia wa Ireland Luke McNally, 24. (Football Insider)
Stoke City inamtaka kiungo wa kati wa klabu ya Blackburn Rovers Muingereza Lewis Travis, mwenye umri wa miaka 26. (Teamtalk)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
8/02/2024 09:39:00 AM
Rating:
