Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Julai, 2024
Mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 23, hana nia ya kuondoka Real Madrid hata kama Manchester City watajaribu kumchukua kama mbadala wa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, ambaye anatazamiwa kujiunga na Atletico Madrid. (AS)
Klabu ya Manchester United wanajiandaa kuwasilisha ofa mpya kwa mlinzi wa Everton, Jarrad Branthwaite, mwenye umri wa miaka 22 baada ya kubaini kuwa mchezaji wao mpya, mlinzi wa timu ya taifa Ufaransa Leny Yoro, 18, hawezi kucheza tena mwaka huu. (Sun)
Beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, na beki wa Morocco Noussair Mazraoui, 26, wanatarajiwa kujiunga na Manchester United kutoka Bayern Munich huku mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yakiendelea. (Sky Sports Germany)
Bayern Munich wamejiondoa katika mpango wa kumsajili beki wa Ujerumani Jonathan Tah, 28 kutoka Bayer Leverkusen. (Kicker)
Crystal Palace wamekataa ofa ya pili, inayoaminika kuwa ya takriban £50m, kutoka kwa Newcastle United kwa ajili ya beki wao Marc Guehi, 24, huku mazungumzo yakiendelea kati ya klabu hizo mbili. (Sky Sports)
Crystal Palace wapo kwenye mazungumzo na Galatasaray kuhusu mkataba wa msimu mzima kwa winga wa zamani wa Eagles Wilfried Zaha. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 31 aliondoka katika klabu ya Selhurst Park na kujiunga na klabu hiyo ya Uturuki kwa uhamisho wa bure msimu uliopita.
Bilionea wa Marekani John Textor ametoa ombi la kuwa mmiliki mkubwa wa Everton, jambo ambalo linaweza kumaliza sakata la kuuzwa kwa klabu hiyo. (Guardian)
Leicester City pia wanashughulikia mpango wa kumsajili Zaha kutoka Galatasaray.
Arsenal wako tayari kuidhinisha kuondoka kwa mshambuliaji Muingereza Eddie Nketiah, 25, kwenda Marseille kwa mkopo na watalazimika kununua kwa ada ya pauni milioni 25. (Athletic)
Klabu ya Wolverhampton Wanderers wanamnyatia winga wa Ajax mwenye umri wa miaka 20 kutoka Ureno Carlos Forbs kuchukua nafasi ya Pedro Neto, 24, ambaye anakaribia kuhamia Chelsea. (Fabrizio Romano)
West Ham United wanakaribia kushinda katika kinyang'anyiro cha kumsajili beki wa Ufaransa Jean-Clair Todibo mwenye umri wa miaka 24 kutoka Nice huku kukiwa na ushindani mkali kutoka kwa Juventus. (Telegraph)
Queens Park Rangers wanavutiwa na kiungo mshambuliaji wa Japan mwenye umri wa miaka 22, Koki Saito, ambaye kwa sasa yuko na klabu ya Lommel ya Ubelgiji. (West London Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 10 Julai, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
8/10/2024 08:27:00 AM
Rating: