Dkt. Charles Mahera amekabidhi ofisi rasmi kwa Naibu Katibu Mkuu mpya
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wa Wizara ya Elimu, Dkt. Charles Mahera, amekabidhi rasmi ofisi kwa Naibu Katibu Mkuu mpya, Dkt. Hussein Mohamed Omar, ambaye ameripoti kazini kufuatia uteuzi wake na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makabidhiano hayo yamefanyika Juni 27, 2025 Jijini Dodoma na kushuhudiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo.
Dkt. Charles Mahera amekabidhi ofisi rasmi kwa Naibu Katibu Mkuu mpya
Reviewed by Zero Degree
on
6/27/2025 01:29:00 PM
Rating:
