Rais Samia amefanya uteuzi mwingine
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi huo ni kama ifuatavyo;
i. Jaji Mkuu mstaafu Prof. Ibrahim Hamis Juma ameteuliwa kuwa Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM). Mhe. Prof. Juma anachukua nafasi ya Mheshimiwa Dkt. Stergomena Lawrence Tax, ambaye ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; na
ii. Dkt. Deo Mwapinga ameteuliwa kuwa Balozi. Dkt. Mwapinga ni Katibu Mkuu wa Wabunge ya Nchi Wanachama wa Mkutano wa Kimataifa wa Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR).
Rais Samia amefanya uteuzi mwingine
Reviewed by Zero Degree
on
6/29/2025 11:10:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
6/29/2025 11:10:00 AM
Rating:

