Tumepambana na tulitaka kushinda mchezo wa leo lakini imeshatokea hivyo - Samatta
Baada ya Taifa Stars kupoteza mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, dhidi ya Niger kwa kichapo cha goli 1-0. Nahodha wa Stars, Mbwana Samatta alisema kuwa hakuna mchezaji ambaye anafurahia matokeo hayo na kuahidi kwamba wanaenda kujipanga kusahihisha makosa yao.
“Kwanza niwapongeze Niger, wametupa mchezo mzuri. Tumejaribu, tumepambana na tulitaka kushinda mchezo wa leo lakini imeshatokea hivyo. Hakuna mchezaji ambaye alikuwa anapenda matokeo ya leo, tayari nimezungumza na wenzangu watakaporudi kwenye vilabu vyao wawe watulivu na kujaribu kusahau haraka kwa kuwa imeshatokea hivyo na hatuwezi kubadilisha matokeo lakini waelewe kwamba tumeanguka na tujipange ili wakati mwingine tutakapokutana tena tusifanye makosa kama ya leo,” - amesema Mbwana Samatta.
Tumepambana na tulitaka kushinda mchezo wa leo lakini imeshatokea hivyo - Samatta
Reviewed by Zero Degree
on
9/09/2025 10:00:00 PM
Rating:
