Loading...

Kwa mara ya kwanza Papa Francis ndani ya Kenya.








Serikali ya Kenya imethibitisha kukamilika kwa maandalizi ya kumpokea kiongozi mkuu wa kanisa katoliki dunia nzima, Papa Francis.
Imebaki siku tatu tu kwa kiongozi huyo wa kanisa kuwasili nchini Kenya, huku viongozi wa kanisa la katoliki nchini humo pia wakithibitisha hilo. 

Papa Francis: "naleta ujumbe wa maridhiano kwa Afrika"

Papa Francis anajianadaa kuanza ziara yake barani Afrika Jumatano wiki hii.

Papa Francis anajiandaa kuanza ziara yake barani Afrika siku ya Jumatano wiki hii inchini Kenya. (REUTERS/Giampiero Sposito)

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani anatarajiwa kuanza ziara yake barani Afrika siku ya Jumatano juma hili.
Nchi yake ya kwanza kuzuru itakuwa ni Kenya kati ya tarehe 25 hadi 27 na serikali ya Nairobi inasema maandalizi yote ya kumpokea kiongozi huyo tayari yamekamilika.
Mamilioni ya watu wanatarajiwa kushiriki misa itakayoongozwa na Papa Francis jijini Nairobi.Siku mbili kabla ya ziara hiyo, Papa Francis ametuma ujumbe wa tumaini kwa watu wa Afrika na kusema anawaletea ujumbe wa amani, msamaha na msamaha.

Hii ni ziara ya kwanza ya Papa Francis barani Afrika, ambapo mbali na Kenya, pia ataitembelea Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Source: BBC


Kwa mara ya kwanza Papa Francis ndani ya Kenya. Kwa mara ya kwanza Papa Francis ndani ya Kenya. Reviewed by Zero Degree on 11/23/2015 11:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.