Loading...

“Hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi tu,...” Soma Kiapo cha jasho walichoapa Mawaziri, wapania kazi kwa kwenda mbele!!

Dar es Salaam. Hafla ya kuapishwa kwa mawaziri iliyofanyika jana Ikulu jijini Dar es Salaam ilikuwa kavu isiyo na shangwe zilizozoeleka huku mawaziri wakionekana wazi kuwa wamepania kufanyia kazi kiapo chao.

Hafla hiyo ilifanyika bila ya kuwapo na viburudisho vya kifahari na shamrashamra nyingine, lakini hilo halikuonekana kuwasumbua mawaziri hao ambao uteuzi wao ulitangazwa juzi, na badala yake wakaeleza jinsi walivyojipanga kutekeleza majukumu yao kwa kasi ya “hapa kazi tu”.

Baadhi ya mawaziri walianza kazi moja kwa moja baada ya kutoka Ikulu, akiwamo Dk Hamisi Kigwangalla ambaye alikwenda moja kwa moja Hospitali ya Amana iliyopo wilayani Ilala na kufanya kikao kifupi na madaktari na uongozi wa hospitali hiyo.

“Nitahakikisha kila Mtanzania anapata huduma nzuri ya afya. Hilo litafikiwa kama tutakuwa na zahanati kila kijiji, dawa za kutosha, vifaa tiba na watumishi sekta ya afya wapate motisha ya kufanya kazi,” alisema Dk Kigwangalla ambaye ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto mara baada ya kuapishwa.

Waziri Mhagama anena
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alielekeza akili yake katika kutekeleza majukumu yake vizuri.

“Hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi tu,” alisema Mhagama. “Nitafanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa, nikiongozwa na uzalendo.”

Waziri huyo, ambaye aliambatana na mwanae, alisema kazi kubwa atakayoifanya ni kulifanya Bunge kuwa la wananchi, kuwaunganisha wafanyakazi, vijana na sekta zote zinazosimamiwa na wizara hiyo.

Awali Mhagama alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Sera, Uratibu na Bunge). Wizara hiyo ilikatwa na kuunganishwa na wizara nyingine mbili.

Alipoulizwa sababu za kurejeshwa tena katika wizara hiyo alisema: “Nimerudishwa sababu nikiwa bungeni nilipunguza tofauti za vyama na kuwatumikia zaidi wananchi. Pia nilikuwa kiunganishi kizuri sana.”

Kilimo na Uvuvi ni maisha ya Watz
Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba, ambaye alikuwa Naibu Waziri wa Fedha (Sera) katika utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne, alisema Rais ametoa dira na hivyo jukumu lake ni kuifuata.

“Kilimo, mifugo na uvuvi ndiyo maisha ya Watanzania na tayari rais ametoa dira ya jinsi ya kuelekea katika mambo hayo. Jukumu nililonalo ni kufuata dira hiyo kuhakikisha wakulima, wavuvi na wafugaji wanakuwa katika mazingira rafiki na kubadili maisha yao,” alisema Nchemba ambaye pia aliomba ridhaa ya CCM kugombea urais.

Kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji, Mwigulu alisema atakalolifanya ni kushirikiana na wizara nyingine ambazo zina uhusiano wa moja kwa moja na matumizi bora ya ardhi.

Mwigulu ambaye aligusia sana suala la kilimo na uvuvi wakati akisaka tiketi ya kupitishwa na CCM kuwania urais, alisema: “Pembejeo za kilimo zinatakiwa kufika kwa wakati, wakulima wasikopwe mazao yao na wapate soko la mazao. Hayo ni mambo niliyoyagusia sana na nitayasimamia.”

Simbachawene atangaza vita

Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala, George Simbachawene alisema katika uongozi wake hataki kuona wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi wakikaa ofisini, na kuwataka kwenda kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatatua.

“Watakaoshindwa kwenda na kazi nitakayoanza nayo, ninawapa pole na wajiandae kutupisha. Ninakerwa kuona watoto wanakaa chini. Tuna miti na misitu ya kutosha, kwa nini watoto wakae chini? Kuanzia mwezi wa sita mwakani, sitaki kuona mtoto anakaa chini. Nawapa miezi sita tu,” alisema

“Watu hawa (wakuu wa wilaya, mikoa na wakurugenzi) wakitekeleza wajibu wao vizuri, matarajio ya Watanzania katika afya, elimu na kilimo yatatimia. Wakuu wa wilaya na mikoa kazi yao si kupokea wageni ni kwenda kuwatumikia wananchi,” alisema.

Nape na sheria za michezo, habari
Nape Nnauye, ambaye ataongoza Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo aliangalia changamoto kwenye sekta zilizo chini yake.

“Sitamuangusha aliyeniamini, walioniamini na Watanzania wote. Katika michezo changamoto ni nyingi, lakini kubwa mbili ni sheria zinazosimamia michezo na nidhamu katika michezo,” alisema.

Alisema masuala hayo yanakwamisha michezo kwa kiasi kikubwa na kutaka ushirikiano na wadau wote wa sekta hiyo.

Nape pia alizungumzia sheria kandamizi kwenye sekta ya habari akisema ataangalia jinsi ya kuzishughulikia ili waandishi waweze kufanya kazi zao kwa uhuru zaidi na kumaliza malalamiko na changamoto mbalimbali.

Dk Possy afurahia kitengo cha walemavu
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wenye Ulemavu, Dk Possy Abdallah alisema kuwa ni jambo la kheri kwa Rais Dk Magufuli kuamua kuweka kitengo kitakachosimamia masilahi ya watu wenye ulemavu na kwamba atafanya kazi kwa kasi licha ya kuwepo changamoto mbele yake.

Dk Possy, ambaye ni mlemavu wa ngozi, alisema mara nyingi masuala ya walemavu yalikuwa yakichukuliwa kiujumla kwa ama kuchanganywa katika idara za maendeleo ya jamii au ustawi wa jamii na kuonekana hayana uzito.

Alisema changamoto zinazowakabili walemavu si nyepesi, hivyo lazima wafanye kazi kwa bidii ili kuhakikisha usawa wa kweli unapatikana kwa kutekeleza Sheria ya Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2010.

“Lakini utekelezaji wake mzuri utahitaji ufanyaji kazi wa sheria nyingine, masuala ya elimu, ajira, afya, hifadhi ya jamii na mengineyo. Tutabadilisha mtazamo juu ya walemavu na ukusanyaji wa mapato,” alisema Dk Abdallah.

Mwalimu kusaka fedha za dawa
Wakati mawaziri wengine wakizungumzia jinsi ya kutatua changamoto hizo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu alisema jambo la kwanza ofisini ni kuhakikisha wanapata fedha za kutosha ili kutatua matatizo hayo, ambayo ni pamoja na upungufu wa dawa, wauguzi, madaktari na wataalamu wengine wa sekta hiyo.

Alisema pia watahakikisha wanaongeza ujuzi wa watumishi wote ili wafanye kazi kwa ufanisi huku wakiwashirikisha zaidi wananchi katika kuboresha sekta hiyo.

Profesa Mbarawa ataka ushirikiano
Akiwa anakabiliwa na kilio kikubwa cha maji, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alisema ili kutatua matatizo hayo ushirikiano na wadau wote ni muhimu ili kufanikisha azma ya usambazaji wa huduma hiyo vijijini na kusadia kukusanya mapato ya kutosha.

Kilio cha maji kilitawala mikutano ya wagombea urais wote wakati wa kampeni na wagombea wote waliahidi kulitatua iwapo wangepewa ridhaa ya kuongoza.

“Tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha tunatatua tatizo la maji na wale wenye tabia ya kukatakata na kuiba maji waache tabia hiyo mara moja,” alisema Profesa Mbarawa.

“Tukifanya hivyo tutapata mapato mazuri na tutaweza kujenga miundombinu ya kisasa ya kusambaza maji na kuzuia yasipotee.”

Lukuvi aonya matajiri wanaopora ardhi 

Naye waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema atafanya kazi kwa ufanisi na kwa kasi zaidi huku akiwatumia salamu vigogo wenye tabia ya kuwanyang’anya ardhi wananchi masikini na wale wanaokwepa kodi ya ardhi kuwa atakabiliana nao. 

“Hawa watu ambao wanavunja sheria mbalimbali za ardhi kwa kujenga kwenye fukwe, sehemu za wazi, mahali pa watu wote wajiandae kutoka tu, wasisubiri nguvu zangu maana yake safari hii nina nguvu zaidi,” alisema Lukuvi.

Waziri Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Ajira na Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angella Kairuki alisema atafanya kazi kwa kasi ya hali ya juu akizingatia utawala bora na maadili, kuboresha nidhamu na kuangalia mifumo ambayo bado haijaboreshwa ili ifanye kazi kwa ufanisi na kwenda na kauli mbiu ya “hapa kazi tu”.

Muhongo, Mwakyembe wazungumza
Mawaziri wawili ambao wamepingwa uteuzi wao kutokana na tuhuma zilizoikumba Serikali ya Awamu ya Nne, Profesa Sospeter Muhongo, ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini, na Dk Harrison Mwakyembe hawakutaka kujikita kujibu mashambulizi dhidi yao.

Profesa Muhongo, ambaye alilazimika kujiuzulu uwaziri wa Nishati na Madini wakati wa kashfa ya escrow takriban mwaka mmja uliopita lakini baadaye akasafishwa na Sekretarieti ya Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma, alirusha swali kuhusu sakata hilo kwa wale wanaomtuhumu.

“Kawaulize hao wanaopinga,” alisema alipotakiwa kueleza anazungumziaje msimamo wa wanasiasa wa upinzani wanaopinga uteuzi wake.

Na hata alipoulizwa anafikiri ni sababu zipi zilizomfanya arejeshwe, alisema: “Kawaulize wanaohoji.”

Lakini akajikita zaidi kuzungumzia majukumu yake akisema ataanza kufanya kazi pale alipoishia.

“Kama tunataka kuondoka katika umasikini ni lazima tuwe na umeme wa uhakika na usio katika katika. Tukitaka nchi yetu iwe na kipato cha kati lazima tuzalishe umeme wa Megawati 10,000 hadi 15,000. Ukiwa na umeme huu nchi itazalisha ajira, bidhaa zitashuka bei na hata bei ya umeme itapungua,” alisema.

Naye Dk Mwakyembe hakutaka kuzungumzia kabisa tuhuma za wapinzani dhidi ya sakata la ununuzi wa mabehewa na badala yake akasema apewe muda ili kupitia masuala mbalimbali kujua sehemu zenye changamoto, huku akisisitiza kuwa kwa kasi aliyoanza nayo Rais Magufuli ni lazima wizara hiyo ijipange na kuwa chachu ya maendeleo ya nchi.



HIZI NI PICHA BAADHI KATIKA TUKIO HILO:



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue


Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani akila kiapo



Mhe. Dkt. Asha-Rose
Mtengeti MIGIRO (Mb) Waziri wa Katiba na Sheria



Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii akila kiapo



Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo



Rais Kikwete akimuapisha Mhe.
Saada Mkuya SALUM (Mb) Waziri wa Fedha



Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akila kiapo



Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo



Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati) akila kiapo



Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji



Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara



Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akila kiapo



Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akila kiapo



Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akiapishwa



Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha akila kiapo


Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii akila kiapo



Mhe. Juma Selemani NKAMIA
(Mb) Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo



Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii


Picha za Kumbukumbu


Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri na manaibu waziri baada ya hafla ya kula viapo



Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Katibu Mkuu Kiongozi wakipozi na mawaziri baada ya kiapo


Picha za Familia

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (Mb)
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.



Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia ya Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb)
Waziri wa Mambo ya Ndani



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Asha-Rose Mtengeti MIGIRO (Mb)
Waziri wa Katiba na Sheria



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Lazaro Samuel NYALANDU (Mb)
Waziri wa Maliasili na Utalii



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Seif Seleman RASHIDI (Mb)
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii



Rais Kikwete na baadhi ya wanafamilia wa Mhe. Saada Mkuya SALUM (Mb)
Waziri wa Fedha



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Dkt. Titus Mlengeya Dismas KAMANI (Mb)
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha



Rais Kikwete na familia ya Mhe. Charles Muhangwa KITWANGA (Mb)
Naibu Waziri (Nishati)



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Amos Gabriel MAKALLA (Mb)
Naibu Waziri wa Maji



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Janet Zebedayo MBENE (Mb)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Jenista Joakim MHAGAMA (Mb)
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Pindi Hazara CHANA (Mb)
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Godfrey Weston ZAMBI (Mb)
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA (Mb)
Naibu Waziri wa Fedha



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Juma Selemani NKAMIA (Mb)
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Mahmoud Hassan MGIMWA (Mb)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii



Rais Kikwete akiwa na familia ya Mhe. Dkt. Kebwe Stephen KEBWE (Mb)
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii



Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali akiwa na baadhi ya mawaziri na naibu waziri waliokula kiapo leo



Rais Kikwete na Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiwa na makamanda na viongozi katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa



Rais Kikwete na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani wakiwa na wakuu wa vyombo vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani

Rais wa awamu iliyopita Jakaya Kikwete akiongea na Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani na wakuu wa vyombo mbalimbali vya dola vilivyo chini ya wizara ya mambo ya ndani



Mhe. Mathias Meinrad CHIKAWE (Mb) Waziri wa Mambo ya Ndani akiwa na viongozi wa vikosi mbalimbali vilivyo chini ya wizara yake



Mhe. Mwigulu Lameck NCHEMBA Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Adam Kighoma Ali MALIMA (Mb) Naibu Waziri wa Fedha na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya fedha.
Credits: Mwananchi




Mshirikishe na mwenzako kuhusu habari hii!!
“Hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi tu,...” Soma Kiapo cha jasho walichoapa Mawaziri, wapania kazi kwa kwenda mbele!! “Hakuna kingine zaidi ya kufanya kazi tu,...”  Soma Kiapo cha jasho walichoapa Mawaziri, wapania kazi kwa kwenda mbele!! Reviewed by Zero Degree on 12/13/2015 01:22:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.