Loading...

Dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa Kilo 7 zakamatwa Tunduma.


Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi

Polisi mkoani 
Mbeya wameanzisha msako wa dawa za kulevya na kuwakamata watu wanne kwa tuhuma za kukutwa na bangi yenye uzito wa zaidi ya kilo saba na heroini katika miji ya Tunduma na Chunya.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi alisema msako huo ulimnasa mwanamke katika mji wa Tunduma akiwa na kilo 7.1 za bangi kwenye mabegi wakati akiingia nchini kutoka Afrika Kusini.

Msangi alisema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 31, alikamatwa katika kituo cha ukaguzi mjini humo alipokuwa akisafiri kwa njia ya barabara kuelekea Dar es Salaam.

Katika tukio la pili, Kamanda huyo alisema polisi walimkamata mkazi wa Mtaa wa Tukuyu mjini humo, akiwa na pipi moja ya heroini.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye msako huo wa polisi unaoendelea mjini humo akiwa na dawa hizo ambazo thamani yake bado haijafahamika.

Mkazi mwingine wa mtaa huo, anashikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na gramu nne za bangi.

“Tumemkamata pia mkazi wa Kijiji cha Bintimanyanga wilayani Chunya akiwa na kete tatu za bangi,” alisema Msangi.

Alisema uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao umekamilika na kwamba watafikishwa mahakamani wakati wowote kujibu mashtaka.

Alisema msako huo hautamuacha yeyote anayejishughulisha na biashara hiyo.



ZeroDegree.
Dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa Kilo 7 zakamatwa Tunduma. Dawa za kulevya aina ya heroini zenye uzito wa Kilo 7 zakamatwa Tunduma. Reviewed by Zero Degree on 1/21/2016 02:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.