Loading...

JK, Majaliwa wamtembelea Sumaye Muhimbili.


Waziri mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye jana, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam. Rais mstaafu, Jakaya Kikwete akiambatana na mkewe Salma, jana walimtembelea Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Muhimbili.

Kikwete ambaye alifika hospitalini hapo saa 11 jioni, alianza kuwasalimia baadhi ya wagonjwa waliolazwa na baadaye kuingia wodi aliyolazwa Sumaye.

Baada ya kuingia katika chumba hicho, Kikwete alikaa kwenye kochi pamoja na Sumaye kisha kumpa pole na kumtania Sumaye aliyekuwa na mkewe Esther kuwa amenenepa japokuwa anaumwa.

Sumaye alisema ana siku ya tano hospitalini hapo na kuelezea furaha yake kwa ujio huo wa Kikwete.

“Japokuwa nilikuwa katika hali mbaya ila sasa hivi naendelea vizuri. Pia, nakupongeza mheshimiwa (Kikwete) kwa kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Sumaye. Mbali na Kikwete, Waziri Mkuu, Kassim majaliwa na mkewe nao walimtembelea kiongozi huyo jana.

Kaimu Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema kila siku hali ya Sumaye inaimarika. Juzi, Rais Magufuli alimtembelea Sumaye na kumpa pole huku akimuombea apone haraka.


Source: Mwananchi
JK, Majaliwa wamtembelea Sumaye Muhimbili. JK, Majaliwa wamtembelea Sumaye Muhimbili. Reviewed by Zero Degree on 1/13/2016 12:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.