Loading...

Kenya yashika nafasi ya 139 duniani miongoni mwa mataifa yaliyo na viwango vya juu vya ufisadi.


Mkurugenzi Mkuu wa Transparency International Kenya, Samuel Kimeu.    

Nairobi. Kenya imeshika nafasi ya 139 duniani miongoni mwa mataifa yaliyo na viwango vya juu vya ufisadi.



Shirika la Transparency International juzi, lilisema kuwa kiwango cha ufisadi kimekuwa kikiongezeka katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Taarifa hiyo ilisema kwamba Rwanda na Tanzania ndiyo mataifa yameibuka kuwa bora katika utekelezaji wa mambo kwa njia ya uwazi kanda ya nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Aidha, shirika hilo lilitoa pendekezo la Serikali kuweka mikakati ya kushirikisha na asasi nyingine kando na EACC kukabiliana na ufisadi nchini humo.

Shirika hilo liliongeza kusema kwamba ipo haja kwa Idara ya Sheria kuharakisha mchakato wa kusikilizwa kwa kesi zinazohusu ufisadi nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa Transparency International Kenya, Samuel Kimeu alisema mchango wa idara hiyo ni muhimu ikiwa ufanisi kamili utapatikana katika vita hivyo.

“Sharti Idara ya Sheria iweze kujizatiti zaidi na kuhakikisha inafuatilia kesi zinazohusu ufisadi,” alisema Kimeu.

Shirika hilo liliongeza kwenye taarifa yake hiyo ya utafiti ikitoa changamoto kwa kusema kuwafahamu wahusika wakuu wanaohusika na ufisadi haitoshi, bali lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.

Shirika hilo lilisema ikiwa nchi itaamua kuwakamata na kuwafikisha mahakamani kisha sheria zikachukuliwa basi hata maendeleo ya nchi yataonekana. Taarifa hiyo ilisema baada ya kukamilisha utafiti huo kwa ujumla, nchi ya Kenya ilipata wastani wa asilimia 25, sawa na ilivyokuwa mnamo 2014.




Source: Mwananchi
Kenya yashika nafasi ya 139 duniani miongoni mwa mataifa yaliyo na viwango vya juu vya ufisadi. Kenya yashika nafasi ya 139 duniani miongoni mwa mataifa yaliyo na viwango vya juu vya ufisadi. Reviewed by Zero Degree on 1/28/2016 01:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.