Loading...

Kuna maisha baada ya uraisi na hakuna haja ya kung'ang'ania baada ya muda wa kikatiba kuisha, Dk. Kikwete.


Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Dk Asha Rose Migiro akimtunukia Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Stashada ya Falsafa ya Heshima wakati wa mahafali ya 30 ya Chuo hicho yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

Dar es Salaam: Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete amesema kuwa kuna maisha baada ya urais na kwamba, hakuna haja ya kung’ang’ania baada ya muda wa kikatiba kumalizika.

Amesema kwamba baada ya kumaliza muda wake amerudi kijijini Msoga kujishughulisha na kilimo.

Kikwete aliyasema hayo jana kabla ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu ya Falsafa ya Heshima ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) katika mahafali ya 30, ikiegemea kwenye masuala ya ushirikiano na uhusiano wa kimataifa.

“Kwa sasa ninaishi vizuri kijijini Msoga, niko na familia yangu ninajihusisha na kilimo,” alisema.

Kiongozi huyo ambaye aliwahi kusema kuwa ana hamu ya kumaliza muhula wake arudi kijijini kulima mananasi, alihitimisha muhula wake Novemba 5, mwaka jana kwa kumkabidhi kijiti Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli.

Akizungumzia shahada hiyo alisema, alikuwa akishiriki masuala mbalimbali ya kimataifa na aliiunganisha Tanzania na mataifa mengine na hiyo ndiyo iliyompa heshima.

Alisema kati ya mambo anayoamini yamempa heshima hiyo ni utatuzi wa migogoro ya kisiasa ya kimataifa ukiwamo ule wa Kenya na Lesotho.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema chuo hicho kimeamua kutoa tuzo hiyo kwa kiongozi huyo kwa kuwa wamekuwa wakiangalia watu waliofanya mambo makubwa katika jamii.

Mwingine aliyepewa shahada ya heshima ni Rais wa Chuo Kikuu cha Chosan kilichopo Korea Kusini, Profesa Chae-Hong Sub.


Source:Mwananchi
Kuna maisha baada ya uraisi na hakuna haja ya kung'ang'ania baada ya muda wa kikatiba kuisha, Dk. Kikwete. Kuna maisha baada ya uraisi na hakuna haja ya kung'ang'ania baada ya muda wa kikatiba kuisha, Dk. Kikwete. Reviewed by Zero Degree on 1/22/2016 12:37:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.