Loading...

Lowassa, Dk Salim wamjulia hali Sumaye.


Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa (kulia) na Salim Ahmed Salim wakisalimiana walipokutana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam jana walipokwenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye (kushoto) aliyelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mkewe, Regina jana walimtembelea Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye anayeendelea kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Muhimbili.

Pia, Waziri Mkuu mstaafu, Dk Salim Ahmed Salim na kada wa Chadema Profesa Mwesiga Baregu, walifika hospitalini hapo jana kumjulia hali Sumaye.

Lowassa aliwasili hospitali hapo saa 6.50 mchana na kutumia dakika 42 kuzungumza na Sumaye. Baada ya kutoka, Lowassa alizungumza kwa kifupi na wanahabari na kusema hatua ya viongozi waandamizi wa Serikali walioko madarakani, waliostaafu na makada CCM kwenda kumuona Sumaye kuwa; “ni jambo jema la kuheshimiana, kujaliana na kutakiana mema.”

Viongozi ambao wameshafika Muhimbili kumjulia hali Sumaye ambaye leo anatimiza siku ya saba, tangu alazwe ni Rais John Magufuli, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete na mkewe Salma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale- Mwiru.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hali ya Sumaye inaendelea kuimarika. 




Source: Mwananchi
Lowassa, Dk Salim wamjulia hali Sumaye. Lowassa, Dk Salim wamjulia hali Sumaye. Reviewed by Zero Degree on 1/14/2016 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.