Loading...

Rais Museveni alikimbia mdahalo.


Wasomi mbalimbali wa Afrika walihoji kitendo cha kiongozi huyo wa nchi kukimbia mdahalo ulioandaliwa kwa ajili ya kusikia sera za wagombea wote wanane wa urais.



Wiki iliyopita wagombea saba walishiriki mdahalo wa pamoja ulioangazia masuala ya uchumi, afya, elimu, demokrasia na maendeleo katika jamii.

Hata hivyo licha ya mdahalo huo kutangazwa na kutolewa taarifa zaidi ya mwezi mmoja kwa wagombea wote Rais wa sasa Yoweri Museveni hakuweza kuhudhuria kwa madai kwamba alikuwa kwenye kampeni zake.

Mdahalo huo ulihudhburiwa na wagombea wengine akiwamo Dk kiiza Besigye ambaye alieleza kukasirishwa kwake dhidi ya waandaaji wa mdahalo akisema waliomdanganya na kumfanya ashiriki wakijua kwamba Rais Museveni atakuwapo.

Moja ya mada iliyosisimua ni kuhusu sekta afya ambapo wengi wa wagombea walisema mfumo wake umeharibika.

Kuhusu kilichopo kwenye mikataba ya Serikali kwa upande wa mafuta hakuna mgombea aliyeonyesha kufahamu zaidi akiwamo Patrick Amama Mbambazi ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya

Museveni.

Wagombea wote walikubali kwamba uchumi wa Uganda uko taabani, ufisadi umekithiri na fedha za serikali zinatumika vibaya.



Source: Mwananchi
Rais Museveni alikimbia mdahalo. Rais Museveni alikimbia mdahalo. Reviewed by Zero Degree on 1/22/2016 12:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.