Serikali yasaka bosi wa Bodi ya Mikopo.
Dar es Salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza nafasi ya kazi ya mkurugenzi mtendaji.
Nafasi hiyo ilitangazwa jana kupitia gazeti la Daily News kwa ajili ya kuziba pengo la mkurugenzi wa sasa, George Nyatega anayetarajiwa kustaafu Agosti.
Miongoni mwa sifa zilizotajwa ni muombaji kuwa na uwezo wa kupanga na kuandaa sera na mikakati kwa ajili ya kuboresha huduma za bodi hiyo na uwezo wa kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato.
Sifa nyingine ni uwezo wa kuisimamia bodi na watumishi wake katika kutekeleza mipango na sera mbalimbali na kusimamia shughuli za kila siku za watendaji wake.
Tangazo hilo pia lilitaja sifa za elimu kuwa ni shahada ya uzamili katika uhasibu, uchumi, biashara na utawala na uzoefu usiopungua miaka minane.
Source: Mwananchi
Serikali yasaka bosi wa Bodi ya Mikopo.
Reviewed by Zero Degree
on
1/12/2016 11:12:00 AM
Rating: