Loading...

TEF walaani vikali kufutwa kwa gazeti la Mawio.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye

Dar es Salaam. Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeshtushwa na kusononeshwa na Serikali kupitia Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kulifuta gazeti la Mawio katika daftari la msajili.[BOFYA HAPA KULISOMA TAMKO HILO].



Akitoa msimamo wa jukwaa hilo jana, Katibu wake, Neville Meena alisema TEF inachukulia hatua hiyo ni aina mpya ya ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Alisema hawatanyamaza wala kukaa kimya kuona vitendo hivyo vikiendelea.

“Serikali zilizopita tulikuwa tukipambana na vitendo vya kufungiwa kwa magazeti kwa muda maalumu, wakati adhabu kubwa iliyowahi kutolewa ilikuwa ni ile ya kufungiwa kwa muda usiojulikana kwa gazeti la Mwanahalisi, kabla ya gazeti hili kurejeshwa kwa umma na Mahakama,” alisema Meena.

Alifafanua kuwa inaonekana dhamira rasmi ya Serikali ni kutumia sheria kandamizi kudhibiti demokrasia na uhuru wa habari.

Meena alisema jukwaa linatoa wito kwa watawala kutafakari upya suala hilo na kuachana na dhamira hiyo isiyokuwa na tija kwa nchi.

“Uamuzi wa kulifuta Mawio hata kama lilifanya makosa umetufikirisha sana, tumetafakari kwa kina na kujiuliza pengine habari zilizoandikwa na gazeti hili zilikuwa hatari kwa kiasi gani kwa nchi hadi kufikiwa uamuzi huo?

Ni magazeti mangapi yatafutwa baada ya Mawio ikiwa Serikali itaendelea na ubabe wa aina hii?,” alihoji Meena. Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda alisema utaratibu uliotumika kulifungia Mawio ni uleule wa matumizi ya sheria kandamizi ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo imekuwa ikipigiwa kelele kwa kipindi cha miaka 20 sasa.


ZeroDegree.
TEF walaani vikali kufutwa kwa gazeti la Mawio. TEF walaani vikali kufutwa kwa gazeti la Mawio. Reviewed by Zero Degree on 1/21/2016 11:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.