Loading...

Umoja wa africa [AU] sasa kuingia BURUNDI Januari 12.

Makamu wa Rais wa Burundi Gaston Sindimwo
Bujumbura, Burundi. Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) wanasubiri mwafaka wa Serikali ya Burundi kwenda nchini humo kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za kuliepusha taifa hilo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Naibu Balozi wa Marekani, David Pressman, alisema hali nchini Burundi kwa sasa ni mbaya na hatari inayowahitaji wajumbe wa Baraza la Usalama kuingilia kati.

Baraza la Usalama lilihimiza kufanywa ziara hiyo baada ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kukataa mpango wa Umoja wa Afrika (AU) kutuma jeshi la kulinda amani ili kusaidia kutuliza ghasia nchini humo.

Taarifa kutoka kwa wajumbe wa baraza hilo ilidai ziara hiyo huenda ikafanyika Januari 15 au 22 ikiwa Serikali ya Burundi itakubali mazungumzo na wanachama wa Baraza la Usalama.

Wiki iliyopita wananchi Burundi walisema wanaamini kuwa uwezekano wa kuongezeka kwa makaburi ya halaiki katika mji huo.

Wakizungumza na redio ya kimataifa ya Ufaransa walisema wanaamini kuna makaburi ya umati mjini humo baada ya mapigano ya Disemba 11.

Taasisi za kijamii na kieneo nazo zilidai kuwa waathirika wa mapigano hayo ni watu 154 na wengine 150 hawajulikani walipo.

Kwa mujibu wa taasisi hizo, hali hiyo inazidi kutia nguvu madai ya kuwapo kwa makaburi ya umati nchini Burundi.

Shahidi mmoja aliviambia vyombo vya habari kuwa aliona kwa macho yake viwiliwili kadhaa katika maeneo tofauti ya vichakani jioni Desemba 11 mwaka jana. Polisi wamekanusha kuwapo kwa makaburi hayo nchini humo.


Source:Mwananchi

Comment & Share this story!!
Umoja wa africa [AU] sasa kuingia BURUNDI Januari 12. Umoja wa africa [AU] sasa kuingia BURUNDI Januari 12. Reviewed by Zero Degree on 1/02/2016 04:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.