Vigogo watatu Bandari wahamishiwa wizarani.
Dar es Salaam. Vigogo watatu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamerudishwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano baada ya kubainika kuchangia upotevu wa maelfu ya makontena yaliyopitishwa katika Bandari ya Dar es Salaam bila kulipiwa ushuru.
Hao ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Peter Gawile; Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano (Tehama), Kalian Charles na Kaimu Mkurugenzi wa Ununuzi, Mashaka Santa.
Hivi karibuni, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa waliibua ufisadi wa jumla ya makontena zaidi ya 14,000 yaliyopitishwa katika Bandari Kavu (ICD) bila kulipiwa ushuru na kuwasimamisha kazi vigogo kadhaa wa TPA na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Profesa Mbarawa alisema: “Kutokana na Bandari kuwa na mpango wa kuiingizia Serikali mapato tumeamua kuwaondoa hao na kuweka wengine, naamini wataziba mianya yote ya udanganyifu uliokuwa ukifanyika.”
Alisema nafasi hizo zimejazwa na Anthony Mbilinyi, anayekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Benitor Kalinga na anayekuwa Ofisa Ununuzi Mkuu, ambao wanatoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Alisema Abdulrahman Bamba atakuwa Mkuu wa Kitengo cha Tehama akitoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Source: Mwananchi
Vigogo watatu Bandari wahamishiwa wizarani.
Reviewed by Zero Degree
on
1/16/2016 11:51:00 AM
Rating: