Loading...

Aliyefiwa na familia katika ajali mbaya ya basi la Simba Mtoto iliyotokea alhamisi azungumza.


Dar es Salaam. “Nipo njia Panda”. Hayo ni maneno aliyoyatamka mwandishi wa habari mwandamizi wa Redio Mlimani, Hamis Dambaya baada ya kufiwa na mkewe, Raya Said, mtoto Nasreen na mama mkwe katika ajali ya basi iliyotokea Alhamis. 

Dambaya alipoteza ndugu hao katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Simba Mtoto lililogongana uso kwa uso na lori katika Kijiji cha Pangamlima wilayani Muheza, Mkoa wa Tanga. Akizungumza nyumbani kwa wazazi wake Tandika wilayani Temeke juzi, Dambaya alisema hakuamini kilichotokea baada ya kupata taarifa za tukio hilo. 

“Ni vigumu kuamini kwa mtu ambaye umezoeana naye na saa chache kabla umauti kuwafika ulizungumza naye. Hadi sasa naweza kusema nipo njiapanda, nilishamzoea mke wangu. Pia, itakuwa vigumu kumsahau mwanangu Nasreen ambaye alikuwa na tabia ya kuchora ukuta kila anaporudi kutoka shule,” alisema Dambaya. 

Kwa mujibu wa Dambaya, familia yake ilikwenda Tanga kuhudhuria msiba wa mjomba wa mkewe ambao yeye aliwahi kuzika na kurudi Dar es Salaam, kisha mkewe kwenda kwa ajili ya kumalizia msiba huo. Miili ya marehemu hao ilizikwa juzi mkoani humo.

Credits: Mwananchi Communications


ZeroDegree.
Aliyefiwa na familia katika ajali mbaya ya basi la Simba Mtoto iliyotokea alhamisi azungumza. Aliyefiwa na familia katika ajali mbaya ya basi la Simba Mtoto iliyotokea alhamisi azungumza. Reviewed by Zero Degree on 2/14/2016 10:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.