Loading...

Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu leo [ Siku Ya Wapendanao ] ili kuokoa maisha ya wahitaji.


Dar es Salaam. Ofisi ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama Kanda ya Mashariki, imewataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kuchangia damu leo ili kuokoa maisha ya wahitaji.

Msemaji wa ofisi hiyo, Rajab Mwenda alisema uchangiaji huo ni mwendelezo wa kampeni ya ukusanyaji damu inayobebwa na kauli mbiu isemayo “Onyesha upendo kwa kujitolea damu”. 

Alivitaja vituo vitakavyohusika katika ukusanyaji damu kuwa ni hospitali za Amana, Sinza na Temeke. 

“Katika kuadhimishwa Siku ya Wapendanao tumeamua kuhamasisha watu kuchangia damu kwa wapendwa wao ambao ni wahitaji, kwani uhai una thamani kubwa zaidi kuliko kitu chochote,” alisema Mwenda. 

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha wanawake 432 kati ya vizazi hai 100,000 nchini hufa kila mwaka kutokana na uzazi na asilimia 80 ya vifo vyao husababishwa na ukosefu wa damu. Alisema katika Mkoa wa Dar es Salaam mahitaji kwa mwezi ni chupa 4,000, lakini zinazopatikana ni 2,000. 

Kitaifa mahitaji ni kati ya chupa 400,000 hadi 460,000.




ZeroDegree.
Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu leo [ Siku Ya Wapendanao ] ili kuokoa maisha ya wahitaji. Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangia damu leo [ Siku Ya Wapendanao ] ili kuokoa maisha ya wahitaji. Reviewed by Zero Degree on 2/14/2016 10:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.