Loading...

Wakulima watakiwa kuchangamkia soko Afrika Mashariki.



Lushoto. Mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi amewataka wakulima wa mbogamboga na matunda kuchangamkia soko la pamoja la Jumuiya Afrika Mashariki (EAC) na kuacha kusubiri walanguzi wa mazao mashambani.

Akizungumza na wakulima wa Mlalo, Bumbuli na Lushoto jana, Shangazi alisema wengi wao wamekuwa mtaji wa matajiri na kurudisha nyuma sekta ya kilimo hicho wilayani humo. 

“Kuna soko la pamoja ambalo limefunguliwa zamani, nashangaa sioni mkulima hata mmoja hapa anayepeleka mazao yake moja kwa moja katika soko linalounda jumuiya hiyo,” alisema. 

Alisema miongoni mwa malengo ya uwapo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuwasaidia wakulima na wajasiriamali kutangaza bidhaa zao na kuuza katika masoko. 

Mkulima wa nyanya na maboga, Shembilu Saleh alisema wengi wao wanashindwa kuwakabili wadudu waharibifu wa mazao, baada ya dawa za kuulia kupanda bei. 

“Tunaomba tusaidiwe katika hili la dawa za kuua wadudu,” alisema.




ZeroDegree.
Wakulima watakiwa kuchangamkia soko Afrika Mashariki. Wakulima watakiwa kuchangamkia soko Afrika Mashariki. Reviewed by Zero Degree on 2/14/2016 11:12:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.