Gari la CRDB laopolewa, mfanyakazi hajapatikana
Gari ndogo mali ya benki ya CRDB tawi la Ifakara likiwa linaopolewa kwenye maji baada ya kutumbukia kufuatia ajali ya kupinduka kwa kivuko cha MV II Kilombero kilichokumbwa na dhuruba ya upepo mkali ikiambatana na mvua januari 27 mwaka huu na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine zaidi ya 35 kunusurika kifo mkoani Morogoro.
Kilombero. Gari la Benki ya CRDB limeopolewa katika Mto Kilombero likiwa na Sh3.5 milioni, huku mfanyakazi wake akiwa hajapatikana.
Gari hilo liliopolewa jana saa nane mchana baada ya kulitafuta kwa siku tano tangu lilipozama Mto Kilombero Januari 27 likiwa katika kivuko cha MV Kilombero II.
Mfanyakazi wa CRDB tawi la Ifakara, Dustan Rwegasira (31) ni miongoni mwa abiria waliokuwamo ndani ya kivuko hicho.
Hata hivyo, jitihada mbalimbali za kukiibua kivuko hicho bado zinaendelea baada ya juzi kutumia mbinu ya kutumbukiza mapipa yaliyojazwa maji kisha kuzamishwa chini ili kukitoa kukwama.
Kazi hiyo inafanywa na timu ya wazamiaji wa Kampuni za M.Divers Limited na May-Marine Go Limited.
Mkuu wa Kikosi cha Uzamiaji na Uokoaji wa Kampuni ya M. Divers Limited, Hafidh Seif alisema: “Hesabu zetu zinakwenda vizuri, yale matangi unayoyaona yanazamishwa baada ya kujazwa maji halafu, yakiwa chini yatageuka maboya kisha yatapanda juu na kivuko hicho na kuvutwa na wenye magari,” alisema Seif.
Seif alisema wanakabiliana na changamoto ya kasi ya maji, lakini wanamshukuru Mungu kazi ya kuondoa maji ndani ya vyumba vya maboya ya kivuko imemalizika salama.
Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Gari la CRDB laopolewa, mfanyakazi hajapatikana
Reviewed by Zero Degree
on
2/03/2016 06:15:00 PM
Rating: