Loading...

Cheyo, Mrema wapingwa kuitetea CCM.

Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha TLP,Augustine Mrema akiwa na John Cheyo (UDP) .

Wasomi na wanasiasa nchini wamekosoa kauli za viongozi wa vyama vya siasa, John Cheyo (UDP) na Augustine Mrema (TLP) walizozitoa katika Mkutano Mkuu wa CCM kinyume na malengo ya vyama vyao.

Katika mkutano huo, Mrema alisema, “CCM msione mkipeta ni kwa sababu ya upendo na ukarimu wenu. Mwaka 2009 nilikuwa mgonjwa ni wewe Jakaya (Kikwete) ulinipeleka India na mke wangu kutibiwa.”

Kadhalika, Cheyo alisema ni vigumu kuiondoa CCM madarakani na kuwa siasa si ugomvi kama ambavyo baadhi ya vyama vya upinzani vimekuwa vikifanya.

“Chama cha Mapinduzi ni kigumu kuking’oa. Huwezi kuing’oa CCM kwa kususia vikao vya Bunge. Siasa siyo ugomvi, siyo uadui,” alisema Cheyo alipopewa nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo.(Soma gazeti la Mwananchi la leo).

ZeroDegree.
Cheyo, Mrema wapingwa kuitetea CCM. Cheyo, Mrema wapingwa kuitetea CCM. Reviewed by Zero Degree on 7/27/2016 09:13:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.