Mnara kumuenzi JK kujengwa Kibaha.
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Pwani, wanapanga kujenga mnara wa kumuenzi Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kulitumikia taifa na chama hicho kwa miaka 10.
Mnara huo unatarajiwa kujengwa Kibaha, mkoani Pwani na wabunge 12 wa chama hicho, ambao pia utawekwa picha yake.
Mpango huo ulitangazwa juzi na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa kwa niaba ya wenzake, katika sherehe ya kumpokea na kumpongeza, Kikwete kwa kustaafu uenyekiti wa CCM baada kukiongoza chama hicho kwa miaka 10 na kukiacha kikiwa salama pamoja na taifa.
Alisema kwa kutambua mchango wa Kikwete kwa chama na taifa, wamemua kujenga mnara huo kwenye jengo la Ofisi ya Mkoa wa Pwani, kama shukrani ya kuwatumikia Watanzania na wana CCM kwa kipindi hicho.
“Tunakushukuru kwa kuliongoza taifa hili vizuri, ungeshindwa wala siyo wewe peke yako bali wananchi wote wa mkoa huu, kwa kutambabua na kuthamini kazi yako, tumeamua tukujengee mnara katika eneo ulilowahi kusimama kutangaza nia ya kuwania urais,” alisema.
Dk. Kawambwa alisema ujenzi huo utaanza hivi karibuni na kwamba watamualika Rais huyo mstaafu kuuzindua.
Akizungumza na mamia ya wanachama na wananchi waliompokea juzi wilayani Bagamoyo akitokea mkoani Dodoma, Kikwete alisema mapokezi hayo yamempa heshima na kuona wanachama wanavyomthamini hasa kazi alizofanya.
Pia alisema anamshukuru Mungu ameiacha serikali katika mikono salama ya Rais John Magufuli na chama kiko imara na kwamba hakiwezi kufa labda itokee miujiza.
“Nawashukuru kwa kunijengea mnaara wa kudumu, safari yangu ya urais ilianzia Kibaha na leo nahitimiashia hapahapa ni faraja kubwa sana,” alisema.

ZeroDegree.
Mnara kumuenzi JK kujengwa Kibaha.
Reviewed by Zero Degree
on
7/27/2016 09:19:00 AM
Rating: