Loading...

Tuzo ya mwanasoka bora Ligi Kuu Tanzania Bara kutolewa leo

MCHEZAJI Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara anatarajiwa kujulikana leo wakati wa utoaji tuzo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas jana ilisema aina 13 ya tuzo zitatolewa leo.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas.

Alisema wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora ambaye mshindi atazawadiwa Sh 9,228,820 na timu zao katika mabano ni Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Juma Abdul (Yanga) na Mohamed Hussein (Simba).

Tuzo ya Kipa Bora ambayo zawadi yake ni Sh 5,742,940, inawaniwa na Aishi Manula (Azam), Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na Deogratius Munishi (Yanga).

 PICHA: Mohamed Hussein [ Simba ].

PICHA: Shiza Kichuya [ Mtibwa Sugar ].

Mchezaji Bora wa Kigeni ambaye atazawadiwa fedha taslimu kama ya kipa bora ni Donald Ngoma (Yanga), Thabani Kamusoko (Yanga) na Vincent Agban (Simba), huku Kocha Bora akizawadiwa Sh milioni nane, ambapo wanaowania ni Hans Van Pluijm (Yanga), Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na Salum Mayanga (Tanzania Prisons).

Wanaowania tuzo ya Mwamuzi Bora ni Anthony Kayombo, Ngole Mwangole na Rajab Mrope, ambao mshindi atapata kiasi cha Sh milioni 5.7, huku Mchezaji Bora Chipukizi akizawadiwa Sh milioni nne, ambapo wanaowania ni Farid Mussa (Azam), Mohamed Hussein (Simba), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).


PICHA: Juma Abdul [ Yanga ].

Pia kutakuwa na zawadi ya Goli Bora la Msimu, wanaowania ni Ibrahim Ajib wa Simba na Amis Tambwe wa Yanga na mshindi atapata Sh milioni tatu.

Zawadi nyingine ni ya timu bingwa itakayopata Sh milioni 81, makamu bingwa Sh milioni 40, mshindi wa tatu sh milioni 29 na mshindi wa nne Sh milioni 23, huku timu yenye nidhamu ikipata Sh milioni 17. Yanga ndiyo bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam imeshika nafasi ya pili, Simba ya tatu na Prisons ya nne.


ZeroDegree.
Tuzo ya mwanasoka bora Ligi Kuu Tanzania Bara kutolewa leo Tuzo ya mwanasoka bora Ligi Kuu Tanzania Bara kutolewa leo Reviewed by Zero Degree on 7/17/2016 11:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.