Loading...

Hatimaye Dk. Mwaka Atiwa nguvuni.

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumtia nguvuni tabibu Juma Mwaka, maarufu Kama Dokta Mwaka, baada ya kumsaka kwa siku kadhaa bila mafanikio.



Jeshi la polisi lilikuwa likitekeleza agizo la Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Hamisi Kigwangalla kuwa tabibu huyo mashuhuri akamatwe kwa kukiuka agizo la serikali la kuacha kutoa huduma za tiba asili na tiba mbadala baada ya kufutiwa kibali na baraza la tiba asili na tiba mbadala, ambao walimkuta na hatia.

Dk. Mwaka alikutwa na hatia ya kukiuka masharti ya sheria ya tiba asili na tiba mbadala ya mwaka 2002, sheria namba 23, ulaghai wa kujiita dokta na kujifanya amesomea tiba ya kisasa kumbe la. Kukutwa na shehena ya dawa za kisasa zaidi ya boksi 200 bila vibali vya mamlaka ya chakula na dawa, TFDA na kukutwa na shehena ya dawa za tiba asili na tiba mbadala kinyume cha sheria, hasa baada ya kufutiwa usajili wa kutoa huduma hizo.

Tabibu Mwaka anashikiliwa na polisi kwa mahojiano katika kituo cha kati.

ZeroDegree.
Hatimaye Dk. Mwaka Atiwa nguvuni. Hatimaye Dk. Mwaka Atiwa nguvuni. Reviewed by Zero Degree on 8/11/2016 10:02:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.