Loading...

Waziri Kigwangalla afanya ziara ya Kushtukiza Katika kliniki ya Fore Plan..., Atoa Saa 24 kwa Polisi Kumkamata Dk. Mwaka.

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kingwangalla ameagiza Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kumkamata tabibu maarufu Juma Mwaka ndani ya saa 24.




Dk. Kigwangalla ametoa amri hiyo leo jijini Dar es Salaam alipokitembelea tena kituo cha Fore Plan kinachomilikiwa na tabibu huyo maarufu kwa jina la ‘Dk. Mwaka.’
Dk. Hamisi Kigwangalla alipokuwa kwenye kliniki ya Dk. Mwaka.

Agizo hilo la kukamatwa kwa Dk Mwaka amelitoa baada ya kufanya ziara ya kushtukiza kwenye kiliniki hiyo iliyopo Ilala Bungoni jijini Dar, ili kufanya ukaguzi akitaka kujua nini kinachoendelea kwenye kliniki hiyo ambayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuwa kampuni.

Ilimlazimu asubiri kupata kibali cha polisi ili kuweza kuingia ndani ya jengo la Dk. Mwaka kufanya ukaguzi huo ambapo amesema amekuta shehena ya dawa za tiba asili licha ya kupigwa marufuku na Baraza la Tiba Asili.

Serikali ilitangaza kukifungia kituo hicho cha afya na vingine vitatu mwezi mmoja uliopita kwasababu zilizoelezwa kuwa ni kutoa huduma kinyume na sheria ambapo kituo cha tabibu Mwaka kilidaiwa kufungiwa kwa mmiliki kujiita daktari badala ya tabibu!


Hata hivyo wiki moja baada ya kuifungia kliniki hiyo kutoa huduma zake, iliendelea kujitangaza kuwa inaendelea kufanya kazi kama kampuni ya ushauri na huduma za kiafya na siyo kliniki tena.

Kutoka jina la awali Fore Plan Clinic ilianza kujitangaza kama Fore Plan Company kitendo ambacho Dk. Kingwangalla amekitaja kuwa ni kinyume na sheria na kuagiza tabibu huyo akamatwe haraka iwezekanavyo.


ZeroDegree.
Waziri Kigwangalla afanya ziara ya Kushtukiza Katika kliniki ya Fore Plan..., Atoa Saa 24 kwa Polisi Kumkamata Dk. Mwaka. Waziri Kigwangalla afanya ziara ya Kushtukiza Katika kliniki ya Fore Plan..., Atoa Saa 24 kwa Polisi Kumkamata Dk. Mwaka. Reviewed by Zero Degree on 8/05/2016 09:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.