Loading...

Januzaj ajiunga na klabu ya Sunderland kwa mkopo akitokea Man U.

Uhamisho huo umemuunganisha na meneja wake wa zamani David Moyes pamoja na wachezaji wenzake, Donald Love na Paddy McNair aliyejiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 5.5 wiki hii.

Januzaj, alikuwa anataka kutoka Old Trafford kabisa lakini klabu hiyo ya United iliamua kumkabidhi kwa klabu hiyo kwa mkopo.

Amesha ifungia mabao matano katika mechi 63 alizoshiriki kwenye klabu ya United.
Mkataba wake na Manchester United utamalika mwaka 2018.

Winga huyo alijiunga na timu ya Borussia Dortmund msimu uliopita kwa mkopo wa miezi minne, lakini alishiriki katika mechi 12 kabla ya kurudi katika timu yake ya Manchester United.


ZeroDegree.
Januzaj ajiunga na klabu ya Sunderland kwa mkopo akitokea Man U. Januzaj ajiunga na klabu ya Sunderland kwa mkopo akitokea Man U. Reviewed by Zero Degree on 8/15/2016 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.