Loading...

Klopp bado hajatosheka na magoli, amewasistiza wachezaji wake kuendelea kutupia zaidi.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amewaambia wachezaji wake kuwa anataka mabao mengi zaidi licha ya kuifunga AC Milan 2-0 katika mchezo wa Kombe la Kimataifa.

Divock Origi na Roberto Firmino walifunga mabao hayo kipindi cha pili mjini California Jumamosi usiku, lakini Daniel Sturridge na Adam Lallana walipoteza nafasi za wazi.

Mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji, Origi alifunga bao lililokataliwa, baada ya Liverpool kufungwa 1-0 na Chelsea Jumatano.

“Nimefurahishwa na kiwango tulichoonyesha, hasa katika kipindi cha kwanza. Tulipasiana na tulifanya hivyo hadi tulipofika langoni kwao. Tulitengeneza nafasi lakini tulishindwa kufunga, haina ubishi kwamba tunatakiwa kutumia nafasi zetu,” amesema Klopp.

James Milner alicheza kama beki wa kushoto katika kikosi cha Klopp kilichotumia Uwanja wa Levi unaotumiwa na klabu ya Santa Clara, wakati nyota mpya Sadio Mane pia akiwa uwanjani.

Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Klopp bado hajatosheka na magoli, amewasistiza wachezaji wake kuendelea kutupia zaidi. Klopp bado hajatosheka na magoli, amewasistiza wachezaji wake kuendelea kutupia zaidi. Reviewed by Zero Degree on 8/02/2016 10:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.