Serengeti Boys yapewa shavu.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye. |
Kauli hiyo ilitolewa juzi Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya mchezo kati ya Serengeti Boys walioibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Afrika Kusini, kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Waziri huyo alifurahishwa na kiwango bora kilichooneshwa na Serengeti Boys na kusema kuwa ataangalia uwezekano kama serikali wa kuunga mkono kwa maandalizi ya mchezo wa mwisho kwa kuwa ndiko kugumu zaidi.
Serengeti ilipata ushindi huo badaa ya kutoka sare ya bao 1-1 na Afrika Kusini mjini Johannesburg, na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1.
Vijana hao sasa watacheza dhidi ya vijana wa Congo Brazzavile walioibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namibia na hivyo kuwaondosha kwenye michuano ya jumla ya mabao 5-1.
Waziri Nape alisema kuna haja ya kuwekeza kwa vijana hao walioonesha mwanga kwa kuwa ndio baadaye watakuwa wanacheza katika timu ya taifa ya wakubwa, Taifa Stars iwapo watatengenezwa kuanzia sasa. Alikipongeza kikosi hicho kwa kucheza kandanda yenye kuvutia na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo.
Suala la kuweka kambi nje ya nchi ni kama limeungwa mkono kwani tayari Rais wa TFF, Jamal Malinzi alitoa ahadi kwa vijana hao kuwa iwapo itaitoa Afrika Kusini wataipeleka timu hiyo kuweka kambi nje ya nchi.
Pia, timu hiyo kabla ya kuvaana katika mchezo wa kwanza dhidi ya Afrika Kusini iliwahi kuweka kambi nchini Madagascar, ikiwa pia ni ahadi ya Malinzi baada ya kuitoa Shelisheli.
Fainali za michuano hiyo zimepangwa kufanyika Madagascar mwakani na endapo Tanzania itafuzu itakuwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo ya vijana.
Mwaka 2005 ilifuzu wakati michuano hiyo ilipofanyika Gambia, lakini ilienguliwa baada ya kubainika kumtumia mchezaji Nourdin Bakari aliyezidi umri.
Source: Habari Leo
ZeroDegree.
Serengeti Boys yapewa shavu.
Reviewed by Zero Degree
on
8/23/2016 10:28:00 AM
Rating: