Shirikisho la Soka Tanzania [ TFF ] lawapiga 'Stop' viongozi Mbeya City, Mwadui na Majimaji kujihusisha na soka kwa miaka 5.
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Sheria na uanachama wa TFF, Eliud Mvela. |
TFF imewafungia kwa miaka mitano kujihusisha na soka vigogo wa timu za Mbeya City, Mwadui na Majimaji.
Vigogo hao wamefungiwa kutokana na kufanya udanganyifu katika usajili wa wachezaji wao, huku wachezaji hao wakilimwa mvua ya mwaka mmoja kila mmoja.
Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa Sheria na uanachama wa TFF, Eliud Mvela aliwataja wachezaji waliofungiwa ni William Lucian, Saidi Mkopi na George Mpole huku viongozi waliofungiwa ni Frank Mfunda wa Mbeya City, George Mbano wa Maji Maji na Ramadhani Kilao wa Mwadui.
Alisema maamuzi hayo yamefikiwa Agosti 18 katika kikao cha Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji chini ya Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Raymond Wawa ambayo iliamua kuwachukulia hatua ya kuwafungia ili kukomesha tabia ya udanganyifu katika usajili.
Akifafanua, Mvela alisema Majimaji ya Songea ambayo ina mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye pia amebainika kuwa ndiye Gerald Mpole wa Majimaji ya Songea amefungiwa kucheza soka kwa mwaka kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo la kufanya udanganyifu kwenye usajili.
Majimaji imeagizwa kutomtumia mchezaji huyo kutoka Kimondo FC.
“Mwadui Shinyanga, mchezaji William Lucian aliyesajiliwa na Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili Mwadui ilhali akiwa hajamaliza mkataba na Ndanda. Mwadui isimtumie mchezaji huyo,” alisema Mvela.
Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Shirikisho la Soka Tanzania [ TFF ] lawapiga 'Stop' viongozi Mbeya City, Mwadui na Majimaji kujihusisha na soka kwa miaka 5.
Reviewed by Zero Degree
on
8/24/2016 10:48:00 AM
Rating: