Arsenal wasahau kuhusu Mustafi, Valencia yamzuia beki huyo.
KLABU ya Valencia imeweka wazi kuwa haina mpango wa kumuuza Shkodran Mustafi msimu huu.
Beki huyu wa kimataifa kutoka Ujerumani amekuwa akihusishwa sana na kujiunga na klabu ya Arsenal wakati huu ambapo Arsene Wenger yuko kwenye mpango wa kuiboresha safu ya ulinzi.
Mwanzoni mwa wiki hii, Wenger alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wako kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la Mustafi, lakini taarifa iliyotolewa na Valencia inaonekana ni tofauti na maneno yake.
Akieleza taarifa hiyo, Kocha wa Valencia, Pako Ayestaran, alisema kuwa hawana mpango wa kumuuza Mustafi kwa sasa, ila watakuwa tayari kuzungumza na klabu itakayokuwa tayari kuvunja mkataba wa beki huyo kwa kulipa pauni mil 42.
“Mustafi hauzwi na atabaki hapa (Valencia). Soko bado liko wazi, hatujui kitakachotokea mbele,” alisema Pako.
Kwenye pambano la kwanza la La Liga, Mustafi aliingia kutokea benchi wakati Valencia ikipokea kichapo cha mabao 4-2 kutoka kwa Las Palmas.
Pia Ayestaran aliweka wazi kuwa beki wa zamani wa Everton, Paco Alcacer, hayuko kwenye mipango ya kuondoka Valencia kama ilivyokuwa kwa Mustafi.
“Kuhusu Alcacer naweza kukupa jibu kama nilivyosena kwa Mustafi, mmiliki wa timu ameshaweka wazi kila kitu,” aliongeza.
“Rais wa klabu ameshasema hadharani kuwa Alcacer na Mustafi hawauzwi na sote tunapaswa kuamini hivyo.”
Katika hatua nyingine, Arsenal wameripotiwa kuanza mazungumzo na beki wa Monaco ya Ufaransa, Marcel Tisserand.
Tisserand, mwenye uwezo wa kucheza kama beki wa kulia pia, ameshawasilisha barua kwa mabosi wa Monaco akiomba kuuzwa.
Pia wametajwa kuiwinda saini ya Jonny Evans, anayekipiga West Brom, lakini ugumu unaonekana ni kwenye kutoa kiasi cha pauni mil 25 ili kumsajili beki wa zamani wa Man united.

Credits: Dimba
ZeroDegree.
Arsenal wasahau kuhusu Mustafi, Valencia yamzuia beki huyo.
Reviewed by Zero Degree
on
8/24/2016 10:36:00 AM
Rating: