Loading...

Benki ya NMB kudhamini mashindano ya Rock City Marathon.

BENKI ya NMB imetoa Sh milioni 10 kudhamini mashindano ya mbio za marathon za Rock City zinazotarajiwa kufanyika Mwanza, Septemba 25.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya benki hiyo mtaa wa Ohio Dar es Salaam jana, Mathew Kasonta ambaye ni mwakilishi wa Kampuni ya Capital Plus International inayoandaa mbio hizo alisema mashindano ya mwaka huu yatakuwa tofauti kwa vile yanashirikisha rika mbalimbali kuanzia watoto, watu wenye ulemavu wa ngozi na vijana.


“Tunaishukuru Benki ya NMB kwa sapoti yao kubwa ambayo ndiyo imefanikisha kufanyika kwa mashindano ya mwaka huu, lakini kitu kikubwa cha kujivunia kwetu nikwamba mashindano ya mwaka huu yatashirikisha umri tofauti tofauti na mbio zitakazokimbiwa ni kilometa 21, 5 kwa walemavu wa ngozi, kilometa 3 kwa wazee na kilometa moja kwa watoto,” alisema Kasonta.

Mwakilishi huyo alisema lengo la kutoa nafasi kwa vijana ni kuandaa wanariadha wa baadaye ambao wataipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano mbali mbali ya kidunia ikiwemo yale ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo 2020.

Alisema mashindano hayo yana historia kubwa kwani ndiyo yaliyowaibua wanariadha nguli nchini akiwemo Suleiman Nyambui mshindi wa medali ya fedha katika mbio za meta 5,000 kwenye Olimpiki na Felix Simbu aliyeshika nafasi ya tano kwenye Olimpiki ya Rio 2016 Brazil.

Sangu aliwataka wanariadha mbalimbali wa Kanda ya Ziwa kujitokeza kujaza fomu zitakazowapa nafasi ya kushiriki mbio za mwaka huu na kutaja maeneo ambayo fomu hizo zinakopatikana kuwa ni Uwanja wa Nyamagana, St. Agustine, CBE, Isamilo International School, kituo cha michezo cha Mallya, Geita Gold Mine vyote vya Mwanza na Shinyanga na kwa upande wa Simiyu wawaone maofisa michezo wa mkoa.

NMB imeanza kudhamini mashindano ya mbio za Rock City tangu mwaka 2009 na kunogesha mashindano hayo ambayo kila mwaka yamezidi kufanya vizuri kwa washindi kujinyakulia zawadi mbalimbali.

Credits: Habari Leo
ZeroDegree.
Benki ya NMB kudhamini mashindano ya Rock City Marathon. Benki ya NMB kudhamini mashindano ya Rock City Marathon. Reviewed by Zero Degree on 9/01/2016 02:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.