Loading...

Dunia kusimama leo kwa dakika 90, ..ni Manchester dhidi ya Arsenal, Mourinho Vs Wenger.

Ahadi ya kocha Arsene Wenger kumpa mkono hasimu wake Jose Mourinho leo kwenye Uwanja wa Old Trafford, kikosi dhaifu cha United kinachosaka kuduwaza mashabiki wao pia wale wa Arsenal ni miongoni mwa matukio ya kimichezo yatakayosimamisha dunia kwa dakika 90.

Matukio mengine ni ligi nyingine kali Ulaya, ambako vumbi litatimka kwenye miji ya Madrid, Dortmund na Milan ambako itajaa upinzani wa aina yake. Klabu mbili za Madrid, Atletico na Real Madrid zitapimana nguvu kwenye mchezo wa Ligi Kuu, La Liga.


Nchini Ujerumani, vinara Bayern Munich wanakuwa wageni wa Borussia Dortmund, ambayo msimu huu imekuwa yenye matokeo tofauti. Kwenye Ligi Kuu ya Italia, vinara Juventus wanakabiliana uso kwa uso na AC Milan kwenye mchezo mwingine unatarajiwa kuwa wenye upinzani mkali.

ZeroDegree.
Dunia kusimama leo kwa dakika 90, ..ni Manchester dhidi ya Arsenal, Mourinho Vs Wenger. Dunia kusimama leo kwa dakika 90, ..ni Manchester dhidi ya Arsenal, Mourinho Vs Wenger. Reviewed by Zero Degree on 11/19/2016 11:18:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.