Loading...

Marekani yashambulia jeshi la Syria kimakosa.

Marekani imekiri kufanya mashambulio mashariki mwa Syria yaliyowauwa makumi kadhaa ya vikosi vya serikali ya Syria vinavyopigana dhidi ya Islamic State (IS).

Muungano unaoongozwa na Marekani unasema kuwa lengo kuu la shambulio hilo ambalo limetajwa kama "kosa " la tarehe 17 Septemba lilikuwa ni kulenga mashambulio hayo katika ngome za Islamic State

Ndege za muungano huo kutoka mataifa ya Uingereza, Marekani, Denmark na Australia zilihusika katika shambulio hilo karibu na Deir al-Zour.

Rais wa Syria Bashar al-Assad alisisitiza kuwa shambulio hilo lililosababisha vifo vingi lilikuwa la makusudi.

Shambulio hilo ambalo jeshi la Urusi linasema kuwa liliwauwa watu wapatao 62, lilisitishwa baada ya Urusi kuifahamisha Marekani kwamba inawalenga wanajeshi wa Syria .

"Katika kisa kama hiki, hatukuweza kufikia kiwango chetu cha haiba tuliyonayo ,na tunaweza kufanya vyema kuliko hili," alisema Luteni Generali katika jeshi la Marekani Jeff Harrigian.

Msemaji wa kituo kikuu Marekani kinachotoa maagizo ya harakati za kijeshi za Marekani katika eneo la mashariki ya kati, amesema kosa la mashambulio hayo ni la "kujutia", na kuongeza kuwa haikuwa makusudi kulenga vikosi vya Syria

"Zilikuwa ni ndege nne zilizoendelea kushambulia ngome za majeshi ya Syria kwa karibu saa nzima, ama kwa muda wa zaidi kidogo ya saa moja ," Rais Assad aliliambia shirika la habari la AP mwezi Septemba.

Msemaji wa wizara ya usalama ya Uingereza alisema katika repoti iliyotolewa Jumanne kwamba uamuzi wa mashambulio hayo karibu na Deir al-Zour ulikuwa "wa nia njema ".

"Tunaafiki ripoti ya muungano na maazimio yake kwamba uamuzi wa kutambua maeneo ya kulenga mashambulio ya Daesh ya wapiganaji wa I-S ulikuwa na sababu ," alisema

" Tusingeweza na hatuwezi kufanya mashambulio ambayo yanafahamika kuwa ya ''vikosi vya utawala wa Syria'' kwa makusudi aliongeza.


Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Marekani yashambulia jeshi la Syria kimakosa. Marekani yashambulia jeshi la Syria kimakosa. Reviewed by Zero Degree on 11/30/2016 10:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.