MO abebeshwa jukumu zito Simba.
SIMBA inataka kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu. Hili liko wazi na ndiyo maana, uongozi wa klabu hiyo umekuwa na mikakati mbalimbali, mojawapo ikiwa ni mkakati wa kumkabidhi timu Mohammed Dewji ‘MO’, si kwa ajili ya umiliki tena, bali ni kwa ajili ya kuwa mdhamini mkuu.
Simba inaendelea kupata neema baada ya mwanachama huyo kumaliza tatizo Simba kwa kuwalipa mishahara pamoja na kutoa fedha za usajili wa baadhi ya wachezaji, ikiwemo waliokuwa wametajwa kumaliza mikataba yao.
Wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba yao ni Jonas Mkude, Said Ndemla na wengine waliokuwepo katika mipango ya kocha mkuu wao, Joseph Omog.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba
zilieleza kwamba, baada ya kukaa pande zote mbili walikubaliana kwanza aingie kama mdhamini mkuu wa klabu wakati mchakato wa kufanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa mfumo wa kuuza hisa ukiendelea kwa utaratibu uliowekwa na Serikali.
Mtoa habari huyo alisema kabla ya kutangaza rasmi MO kuingia mkataba wa udhamini, uongozi utaitisha kikao kwa ajili ya kufanya mabadiliko na kuboresha katiba yao.
“Unajua hivyo vyote anavyotoa MO havipo katika mchakato huo wa hisa, bali ni ahadi yake aliyotoa kwa Wanasimba kama mwanachama, licha ya kulipa mishahara hiyo, pia kuna basi la kisasa limeagizwa kwa ajili ya timu hiyo,” alisema.
Mtoa habari huyo alisema hatua ya MO kuichukua Simba kama mdhamini inakuja baada ya timu hiyo kucheza Ligi hiyo bila kuwa na mdhamini, kufuatia kumalizika kwa mkataba uliokuwepo kati ya timu hiyo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Credits: Bingwa
ZeroDegree.
MO abebeshwa jukumu zito Simba.
Reviewed by Zero Degree
on
11/18/2016 12:35:00 PM
Rating: