Loading...

FA yatoa adhabu hii kwa klabu za Chelsea na Manchester City baada ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji.

Chelsea wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wakapigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya EPL.

Katika mechi hiyo iliyochezwa Etihad ilipokaribia kumalizika wachezaji walipishana kauli baada ya Sergio Aguero wa City kumchezea rafu mlinzi David Luiz hali iliyosababisha ugomvi, kabla ya mwamuzi kuwatoa nje Aguero na Fernandinho kwa kadi nyekundu.

Fernandinho alitolewa baada ya kumkaba koo kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas. Awali Chelsea walitahadharishwa kuwa wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.


Vinara hao wa EPL ambao katika mchezo huo walishinda mabao 3-1, wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.

ZeroDegree.
FA yatoa adhabu hii kwa klabu za Chelsea na Manchester City baada ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji. FA yatoa adhabu hii kwa klabu za Chelsea na Manchester City baada ya kushindwa kuwadhibiti wachezaji. Reviewed by Zero Degree on 12/14/2016 03:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.