Kampuni ya TBL yaibuka kidedea tena tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeibuka kuwa mshindi wa jumla wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016 inayotolewa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE).Ushindi huu imeupata kwa mara ya pili tena ambapo pia mwaka jana ilikuwa mshindi wa tuzo hii ambayo inatambua taasisi inayotekeleza vigezo vya Raslimali Watu kwa viwango vinavyotakiwa.
Hivi karibuni pia TBL ilishinda tuzo ya mwajiri bora ngazi ya kimataifa kutoka taasisi ya kimataifa ya The Top Employers’ Institute yenye makao yake makuu nchini Uholanzi ambayo inaanda tuzo bora kwa makampuni yanayotekeleza vigezo vya Raslimali Watu kwa viwango vya juu duniani.
Mbali na kushinda tuzo kubwa za uajiri bora ,TBL pia mwaka huu inashikilia ushindi wa jumla wa tuzo ya Rais ya Mzalishaji bora wa mwaka 2015 (President’s Manufacturer of the Year Award (PMAYA).
Mgeni Rasmi katika hafla ya utoaji wa tuzo hizi kwa makampuni katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere International Convention Centre alikuwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa Kassim ambaye alisema kuwa serikali itashirikiana na sekta binafsi kwa kuzijengea mazingira bora ya kufanya biashara ili ziweze kukuza wigo wa ajira kwa wananchi hususani vijana wenye taaluma mbalimbali wanaohitimu masomo yao ya elimu ya juu.

Mkurugenzi wa ATE, Dk.Aggrey Mlimuka, akimpongeza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa TBL Group, David Magese kwa ushindi. |
Wafanyakazi wa TBL Group wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuibuka washindi wa jumla wa tuzo ya mwajiri Bora 2016. |
Wafanyakazi wa TBL Group wakifurahia ushindi wa mshindi wa jumla wa Tuzo ya Mwajiri Bora 2016. |
ZeroDegree.
Kampuni ya TBL yaibuka kidedea tena tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016.
Reviewed by Zero Degree
on
12/10/2016 12:18:00 PM
Rating: