Loading...

Kocha George Lwandamina abatizwa jina jipya na wanajangwani.

KOCHA George Lwandamina kule katika klabu yake ya zamani ya Zesco, alikuwa akijulikana kwa jina la utani la Chicken, lakini wachezaji wa Yanga wamesema hilo wao hawalitambui badala yake wakaamua kumpachika ‘Kubwa la Maadui’

Wachezaji wameshudiwa wakitumia jina la Kubwa la Maadui badala ya Lwandamina pale walipokuwa wakipeana maelekezo yaliyotolewa na kocha huyo.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo alipohojiwa ili kujua kisa cha kumwita jina hilo, ambaye alisema Lwandamina amekuwa akiogopwa na kila mtu.

“Kubwa la Maadui lina maana kuwa ndiye mtu wa mwisho kwa kila kitu na anaweza kutoa amri yoyote pasipo kuhofia chochote na kikatekelezwa.

“Ukiangalia kwenye kikosi chetu kwa sasa kocha hata akikohoa, mchezaji anaanza kuhisi ameitwa au kuna kosa amefanya na muda wowote anaweza kukwambia uruke kichura chura au upige pushapu,” alisema mchezaji huyo.


ZeroDegree.
Kocha George Lwandamina abatizwa jina jipya na wanajangwani. Kocha George Lwandamina abatizwa jina jipya na wanajangwani. Reviewed by Zero Degree on 12/10/2016 11:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.