Loading...

Lwandamina awatuliza Yanga.

Baada ya kichapo cha bao mbili kwa sifuri kocha mkuu wa Yanga, George Lwandamina, asema kwamba hakuwa na malengo ya kupata ushindi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Lwandamina ameondoa fikra za mashabiki wengi waliohitaji kuona Yanga ikiibuka na ushindi, kwani kocha huyo hakuhitaji matokeo ya kuwafurahisha wao zaidi ya kuangalia uwezo wa kila mchezaji.

Mchezo huo uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Yanga walipoteza kwa kufungwa mabao 2-0

Akizungumza na waandishi wa habari, Lwandamina alisema mchezo huo uliandaliwa kwa ajili ya kufanyia kazi upungufu wa wachezaji wake baada ya kuwapigisha tizi la siku 12.

Lwandamina alisema alihitaji mchezo huo ili aweze kupata kikosi bora chenye ushindani kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema anataka kufanya kazi na wachezaji wanaoelewa, hivyo kabla ya kuamua nani anamhitaji ni lazima ajue uwezo wa kila mchezaji.

“Yanga ni timu nzuri wanaweza kucheza soka zuri tulifanya makosa, lakini ukiangalia kikosi kilichocheza kipindi cha kwanza utaona wachezaji wengi si wale wa kikosi cha kwanza cha kocha mwenzangu aliyenitangulia, lengo langu lilikuwa ni kutoa nafasi kwa kila mchezaji na si kupata ushindi,” alisema Lwandamina.

Alisema mchezo huo umempa taswira kuwa nani anaweza kufanya kazi nzuri na yeye, kwani tangu mwanzo aliweka wazi aina ya soka analohitaji.

Lwandamina alitumia vikosi viwili katika mchezo huo, ambapo kikosi cha kwanza kiliundwa na Ally Mustapha ‘Barthez’, Hassan Ramadhan ‘Kessy’, Oscar Joshua, Nadir Haroub Cannavaro, Pato Ngonyani, Juma Said ‘Makapu’, Obrey Chirwa, Malimi Busungu, Anthony Matheo, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya.

Kikosi cha pili kilikuwa hivi; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Vincent Andrew, Simon Msuva, Vincent Bossou, Thaban Kamusoko, Justin Zulu, Donald Ngoma, Amis Tambwe na Deus Kaseke.

ZeroDegree.
Lwandamina awatuliza Yanga. Lwandamina awatuliza Yanga. Reviewed by Zero Degree on 12/12/2016 01:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.