Loading...

Mchezaji bora Afrika mwaka 2017 kujulikana leo.

FAINALI ya tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika inayotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), zinatarajiwa kufanyika leo Jumatatu jioni.

Wachezaji watano walioingia kwenye hatua ya fainali ambao walipigiwa kura na mashabiki wa soka ni pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Riyad Mahrez, Sadio Mane na Yaya Toure.

Mshambuliaji wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon, Aubameyang ndiye anayetajwa kuongoza kwa kura nyingi huku nyota wa Ghana na West Ham, Andre Ayew, akiwa ni wa pili jambo linalotoa nafasi kubwa kwa mmoja kati ya wachezaji hao kutwaa tuzo hiyo.

Mshambuliaji wa Leicester City na timu ya taifa ya Algeria, Mahrez hakuwahi kuingia kwenye tuzo lakini Msenegali ambaye pia anakipiga katika kikosi cha Liverpool, Mane alikuwepo kwenye tuzo za mwaka jana lakini mshindi mara mbili ya tuzo hizo, Toure anayekipiga katika kikosi cha Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast akitarajiwa pia kutoa upinzani mkali dhidi ya wenzake.

ZeroDegree.
Mchezaji bora Afrika mwaka 2017 kujulikana leo. Mchezaji bora Afrika mwaka 2017 kujulikana leo. Reviewed by Zero Degree on 12/12/2016 02:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.