Dawa ya waharibifu wa Viti vya Uwanja wa Taifa yapatikana.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametimiza ahadi yake ya ufungwaji wa kamera za ulinzi (CCTV) kwenye uwanja wa Taifa na kuhimiza zianze kutumika kwenye mechi mbalimbali ili kuwabaini waharibifu wa miundombinu.
Nape alitoa agizo hilo jana alipotembelea kukagua viti vilivyovunjwa na mashabiki wa Simba katika mechi yake dhidi ya Yanga Oktoba mwaka huu na kukagua ufanisi wa kamera 119 za kufuatilia matukio yote uwanjani.
Alisema kazi ya kubaini waharibifu wa miundombinu kwa sura katika uwanja huo kwa kutumia kamera hizo utasaidia kuongeza hali ya usalama kwenye uwanja na pia kusaidia kufuatilia matukio ya kihalifu uwanjani kama vile kuvunja viti.
“Kwa sasa uwanja wetu utaweza kushughulika na mtu mmoja mmoja anayehujumu miundombinu yetu, kwa sababu kamera zetu zina uwezo mkubwa wa kumtambua mtu kwa sura pindi awapo uwanjani kuanzia magetini,” alisema.
Ufungwaji wa kamera hizo ni ahadi ya Waziri Nape aliyowahi kuitoa baada ya mashabiki wa Simba na Yanga kuvunja viti na milango ya mageti kwenye mechi yao ambapo alisema atafunga kamera ili kumbaini mtu mmoja mmoja na kuwachukulia hatua za kisheria badala ya klabu kuadhibiwa.
Aidha, Kaimu Meneja wa uwanja huo Julius Mgaya alitoa taarifa ya maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo unaofanywa na serikali, ambapo alisema kabla ya kuanza kwa michuano ya ligi watakuwa wamemaliza.
Hata hivyo, Waziri alitaka ukarabati ufanyike haraka na kukabidhiwa uwanja huo kesho siku hiyo ndiyo itafahamika thamani ya ukarabati uliofanyika kwa ujumla.

ZeroDegree.
Dawa ya waharibifu wa Viti vya Uwanja wa Taifa yapatikana.
Reviewed by Zero Degree
on
12/12/2016 01:54:00 PM
Rating: