Loading...

Tanzania kuungana na Taifa la Brazili kuomboleza vifo vya wachezaji waliopata ajali ya ndege.

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa(FIFA),limelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ,kama wadau wake kuhakikisha wachezaji wanafunga vitambaa vyeusi kwenye mechi mbali mbali linazozisimamia kama ishara ya kuomboleza vifo vya wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil waliofariki katika ajali ya ndege.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas, alisema jana kuwa FIFA imewataka nchi wanachama wake kuhakikisha wachezaji wanafunga vitambaa vyeusi kama ishara ya kuomboleza msiba huo uliolikumba taifa la Brazil.

“FIFA wametutaarifu sisi kama wanachama wao kuwaelekeza a wechezaji wetu kujumuika nao katika maombolezo kwa kufunga vitambaa vyeusi watakapokuwa wakati wa mechi ,na kwakufanya hivyo tutakuwa pamoja na nchi zingine duniani katika maombolezo hayo”alisema Lucas.

Msafara wa timu ya Chapecoense ulipata ajali ndege Novemba 28 mwezi uliopita ukiwa unaelekea mjini Medeline nchini Colombia kwaajili ya mechi ya michuano ya Copa Sudaamericana,ambapo watu 76 walifariki.

Mechi hiyo ya mkondo wa kwanza ilipangwa kuchezwa katika Uwanja wa Atanasio Girardot kabla ya timu hizo kurudiana nchini Brazil.

Kutokana na ajali hiyo mechi hiyo haikufanikiwa kufanyika.

Tukio hilo la kusikitisha limeikumbusha dunia ajali nyingine zilizowahi kutokea miaka ya nyuma zikizikumba misafara ya timu za soka ambazo ni timu ya Taifa ya Zambia ‘Cipolopolo’,timu ya Manchester United ya England na timu ya Torino ya Italia.

ZeroDegree.
Tanzania kuungana na Taifa la Brazili kuomboleza vifo vya wachezaji waliopata ajali ya ndege. Tanzania kuungana na Taifa la Brazili kuomboleza vifo vya wachezaji waliopata ajali ya ndege. Reviewed by Zero Degree on 12/03/2016 12:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.