Loading...

Arsene Wenger kuadhibiwa na FA kwa vitendo vya utovu wa nidhamu

Chama cha Soka cha Uingereza (FA) kimesema kimemkuta na kosa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa kumfanyia vitendo visivyo vya kinidhamu mwamuzi wa akiba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Arsenal na Burnley.

FA imesema katika mchezo huo uliomalizika kwa Arsenal kushinda goli 2-1, Wenger alimsukuma mwamuzi wa akiba, Anthony Taylor jambo ambalo haliruhusiwi na zaidi akiwa tayari ameshatolewa na mwamuzi katika eneo la benchi la ufundi.



“Arsene Wenger ataadhibiwa kwa vitendo vya utovu wa nidhamu katika mchezo wa Burnley uliochezwa Jumapili [Januari 22, 2017],” ilisema sehemu ya taarifa ya FA na kuongeza.

“Kosa hilo alilifanya katika dakika ya 92. Alitumia lugha ya matusi na isiyopendeza kwa mwamuzi wa akiba, Na zaidi alifanya kosa akiwa tayari ameshatolewa katika eneo lake, mpaka saa 10 jioni, Januari 26, 2017 adhabu itakuwa imeshatolewa.”

ZeroDegree.
Arsene Wenger kuadhibiwa na FA kwa vitendo vya utovu wa nidhamu Arsene Wenger kuadhibiwa na FA kwa vitendo vya utovu wa nidhamu Reviewed by Zero Degree on 1/24/2017 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.