Chapecoense yatangaza kusajili wachezaji 20 wapya, baada ya pigo walilopata katika ajali ya ndege.
- AJALI: Nyota wa soka nchini Brazil afariki Dunia baada ya kumpigia simu mkewe.
- Timu iliyopata ajali ya ndege yatunukiwa kombe la Copa Sudamericana.
Klabu ya Chapecoense nchini Brazil, ambayo iliwapoteza wachezaji wengi kwenye ajali ya ndege Novemba, imetangaza kwamba itawanunua wachezaji 20 wapya wa kucheza msimu ujao.
Wachezaji walionusurika ajali hiyo hata hivyo watahifadhiwa nambari zao za jezi.
- Sababu zilizosababisha kuanguka kwa ndege ya wanasoka Brazil.
- Hizi ndizo ajali za Ndege zilizosababisha vifo vya wachezaji wengi zaidi Duniani.
Shabiki wa soka Brazil akitoa heshima zake kwa wachezaji waliofariki |
Klabu hiyo baadaye ilitunukiwa kikombe hicho na wapinzani wao kutoka Colombia Atletico Nacional wakapewa tuzo ya uchezaji haki.
"Sasa tunalazimika kutumia mikopo," mkurugenzi wa soka Rui Costa alisema.
Beki wa kati Neto na mkabaji kamili Alan Ruschel walinusurika na Costa amesema wanatarajia wachezaji hao watarejea na kuvalia jezi zao.
Kipa wa akiba Jackson Follmann pia alinusurika lakini amekatwa sehemu ya mguu wake.
Chapecoense watacheza mechi yao ya kwanza 26 Januari kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Joinville.

ZeroDegree.
Chapecoense yatangaza kusajili wachezaji 20 wapya, baada ya pigo walilopata katika ajali ya ndege.
Reviewed by Zero Degree
on
1/04/2017 05:12:00 PM
Rating: