Loading...

Donald Trump amteua mkwewe kuwa mshauri mkuu wa Ikulu nchini Marekani.

Jared Kushner na mke wake
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua mkwe wake Jared Kushner, kuwa mshauri mwandamizi wa Ikulu ya nchi hiyo.

Kushner mwenye umri wa miaka 35 ambaye amemuoa binti mkubwa wa Trump, Ivanka, alifanya kazi kubwa wakati wa kampeni za uchaguzi, zilizomuwezesha Trump kushinda.

Jared Kushner akiwa na mke wake, Ivanka Trump.
Majukumu ya kazi yake yanatarajiwa kuhusika na masuala ya sera za nje na ndani ya nchi, ikiwemo masuala ya biashara na Mashariki ya Kati.

Uteuzi huo hauhitaji kuthibitishwa na bunge la seneti.
Lakini hata hivyo baadhi ya wachambuzi wanahoji kama uteuzi huo utakiuka sheria ya kupinga upendeleo wa undugu katika ajira.

Jared Kushner hata chukua mshahara kwa uteuzi huo wa Ikulu ya Marekani na itampa nafasi ya kumfanya kuwa huru na maslahi ya shughuli zake za kibiashara.

ZeroDegree.
Donald Trump amteua mkwewe kuwa mshauri mkuu wa Ikulu nchini Marekani. Donald Trump amteua mkwewe kuwa mshauri mkuu wa Ikulu nchini Marekani. Reviewed by Zero Degree on 1/10/2017 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.