FIFA kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki Kombe la Dunia hadi kufikia nchi 48
Ujerumani ndio mbingwa watetezi wa kikombe hicho walichoshinda nchini Brazil mwaka 2014 |
Shirikisho la Soka Duniani Fifa linatarajiwa kupiga kura leo kuamua kuhusu mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48.
Mpango huo ukiidhinishwa, basi utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na utafaidi Afrika na Asia.
Mpango huu umekuwa ukipigiwa debe na rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino.
Mswizi huyo, ambaye anasema ana uungwaji mkono mkubwa, anataka michuano hiyo iwe na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi.
Klabu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya muondoano.
Iwapo mpango huo utaidhinishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998.
Kuna mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 litaangazia.
Kombe la Dunia lenye timu 48 na makundi 16 ya timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya muondoano ya timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
Kombe la Dunia la timu 48, mechi moja ya muondoano wa kufuzu ambapo mshindi atajiunga na timu 16 nyingine (mechi 80 kwa jumla - 16 za muondoano wa kufuzu na 64 za michuano kamili).
Kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (makundi 76).
Kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88).
Kusalia na Kombe la Dunia lilivyo sasa ambapo kuwa timu 32 (mechi 64).
Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo.
Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.

Rais wa Fifa Gianni Infantino anataka mataifa 48 yashiriki |
Chini ya mpango wa Infantino anaoupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32.
Taifa halitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa.
Udhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha klabu zinazotoka sare kwenye makundi.
Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia na idadi ya Timu kwa miaka iliyopita:

- 1930 nchini Uruguay, Timu 13
- 1934 nchini Italy, Timu 16
- 1950 nchini Brazil, Timu 13
- 1954 nchini Switzerland, Timu 16
- 1958 nchini Sweden, Timu 16
- 1974 nchini West Germany, Timu 16
- 1982 nchini Spain, Timu 24
- 1986 nchini Mexico, Timu 24
- 1998 nchini France, Timu 32
ZeroDegree.
FIFA kuongeza idadi ya nchi zinazoshiriki Kombe la Dunia hadi kufikia nchi 48
Reviewed by Zero Degree
on
1/10/2017 12:28:00 PM
Rating: