Loading...

Kiungo wa zamani wa Ufaransa, Claudio Makelele apata shavu Klabu ya Swansea

Klabu ya Swansea City imemuajili aliyekuwa kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Chelsea Claudio Makelele kuwa kocha msaidizi.

Makelele ambaye ana umri wa miaka 43 amesaini mkataba ambao utaishia mwisho wa msimu huu.

Makelele anajiunga tena na kocha Paul Clement ambaye alifanya kazi naye akiwa mchezaji wa Chelsea kutoka mwaka 2007-2008 pamoja na akiwa kocha msaidizi wa PSG chini ya meneja Carlo Ancelotti.

”Nimefurahi sana kuwa hapa na kufanya kazi na Swansea, alisema Makelele. Paul ni mshauri wangu. Amenifunza mengi wakati nilipofanya kazi naye. Niliposikia kwamba alirudi katika ligi ya Uingereza nilimpigia simu na kumuuliza iwapo naweza kumsaidia kaklabu ya Swansea”.

Makelele atakuwa katika mechi ya Swansea dhidi ya Arsenal.

ZeroDegree.
Kiungo wa zamani wa Ufaransa, Claudio Makelele apata shavu Klabu ya Swansea Kiungo wa zamani wa Ufaransa, Claudio Makelele apata shavu Klabu ya Swansea Reviewed by Zero Degree on 1/13/2017 05:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.