Loading...

Safu ya uongozi katika Jeshi la Magereza yafanyiwa mabadiliko.

Kaimu Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi siku chache baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli.

Kamishna Malewa aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo baada ya Rais Magufuli kukubali na kuridhia kusitisha mkataba wa kustaafu kwa John Minja Desemba 2, mwaka jana.

Katika panga pangua hiyo ya Dk Malewa, baadhi ya vigogo wa jeshi hilo wameshushwa vyeo vya madaraka huku baadhi wakihamishwa vituo vyao vya kazi.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ofisa Habari wa Magereza, Lucas Mboje imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida na yanalenga kuboresha utendaji kazi na ufanisi wa jeshi hilo.

ZeroDegree.
Safu ya uongozi katika Jeshi la Magereza yafanyiwa mabadiliko. Safu ya uongozi katika Jeshi la Magereza yafanyiwa mabadiliko. Reviewed by Zero Degree on 1/08/2017 10:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.