Loading...

Tangu kutokea kwa ajali ya ndege, ..hatimaye Chapecoense wacheza mechi yao ya kwanza

Timu ya Chapecoense ya nchini Brazil ilipata ajali ya ndege Novemba 28.Katika ajali hiyo iliyoua watu 71 ambapo kati ya hao 71 kulikuwa na wachezaji 19.Timu hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Colombia kucheza faini ya kombe la Copa Sudamericana.

Sasa kwa mara ya kwanza timu ya Chapecoense imecheza mechi yake ya kwanza toka ajali hiyo itokee.Chapecoense walicheza mchezo huo jana dhidi ya Palmeiras katika uwanja wao wa nyumbani wa Arena Conda.



Katika mechi hiyo Chapecoense ambayo walilibeba kombe lao walilopewa pamoja na medali.Katika mechi hiyo wachezaji wa Chapecoense walikuwa katika hali ya huzuni haswa baada ya kujitokeza uwanjani wachezaji wao ambao walisalia katika tukio hilo.
Wachezaji wa Chapecoense Neto,Jackson Follman na Alan Ruschel ambao walisalimika katika ajali hiyo walikuwepo uwanjani hapo.Chapecoense walipewa kombe hilo na timu ya Atletico Nacional baada ya ajali hiyo.


Klabu ya Chapecoense wachezaji wengi msimu huu wamewachukua kwa mkopo ili kuijenga upya timu yao.Dakika ya 11 tu Chapecoense walifungwa goli la kwanza baada ya Raphael Veigas kuipatia Palmeiras goli.Lakini iliwachukua dakika tatu Chapecoense kusawazisha goli hilo kupitia Douglas Grolli aliyepo kwa mkopo klabuni hapo kutokea Cruziero.

Chapecoense waliongoza katika mechi hiyo baada ya Amar ambae alicheza dhidi ya rimu ya wazazi wake kuipatia Chape goli la pili.Lakini dakika ya 78 Palmeiras walisawazisha goli hilo.

Mchezo huo ulisimama dakika ya 71 ambapo watu wote uwanjani walisimama na kutoa heshima kwa waliokufa.Kusimama kwa mechi dakika ya 71 kulitokana na kukumbuka wahanga ho ambao idadi yao ilikuwa 71.


Nusu ya mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo yatapelekwa kwa familia za wahanga huku nusu nyingine ikitumika kuitengeneza timu.

ZeroDegree.
Tangu kutokea kwa ajali ya ndege, ..hatimaye Chapecoense wacheza mechi yao ya kwanza Tangu kutokea kwa ajali ya ndege, ..hatimaye Chapecoense wacheza mechi yao ya kwanza Reviewed by Zero Degree on 1/22/2017 01:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.