Loading...

Conte atoa sababu ya kumwanzisha Fabregas kipindi cha kwanza

Ilikuwa mchezo wake wa 300 kwa Fabregas kuonekana ndani ya Ligi kuu ya Uingereza katika kipindi cha kazi yake ya soka.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa katika kikosi cha kwanza pamoja na N'Golo Kante wakati huo Conte akimuacha Nemanja Matic benchi.

Kocha wa huyo wa Chelsea amesisitiza kuwa Fabregas amekuwa na hari nzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kimiliki nafasi yake baada ya wiki ya nzima ya mazoezi.

Aliwaambia Sky Sports kwamba: "Baada ya wiki moja ya kazi, hua najaribu kila mchezo na kuchukua uamuzi bora kwa timu kulingana na mpinzani ambaye tunaenda kukutana naye.

"Najua ninaweza kuwategemea hawa wachezaji.

"Na kwa upande wagu mimi, katika kila mchezo inanipasa kuchukua uamuzi bora."
Conte atoa sababu ya kumwanzisha Fabregas kipindi cha kwanza Conte atoa sababu ya kumwanzisha Fabregas kipindi cha kwanza Reviewed by Zero Degree on 2/26/2017 05:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.